Tuesday, November 6, 2012

WAZO LA LEO

Mpaka sasa nani unahisi atanyakuwa kitita cha milioni 50? Kumbuka kumpigia kura mshiriki umpendae mara nyingi uwezavyo...... Jumanne nje!


Thursday, October 25, 2012

WAZO LA LEO



"Kila jambo tunalokumbana nalo katika maisha, hata kama ni baya vipi, jambo hilo linatokea katika maisha yetu kutufunza kitu." - Iyanla Vanzant

Wednesday, October 24, 2012

WAZO LA LEO


"Mtu akikuonyesha yeye ni nani, muamini mara hiyo ya kwanza" - Maya Angelou

Monday, October 15, 2012

MUONEKANO WANGU KATIKA MAJARIDA TOFAUTI

Pata fursa ya kuangalia muonekano wangu katika majarida tofauti niliyowahi kufanya nao mahojiano.








WAZO LA LEO

"Hamna mtu atakayekupenda zaidi ya unavyojipenda wewe mwenyewe"

Friday, October 5, 2012

WAZO LA LEO

"Kama hupendi kitu, badilisha. Kama hutofanikiwa kukibadilisha, badilisha mtazamo wako. Si kulalamika." – Maya Angelou

Tuesday, October 2, 2012

KANGA NA MAANDISHI YAKE

Maandishi ya kanga huwa yananifurahisha sana. Kama Mtanzania, najivunia sana utamaduni huu na muendelezo wa kudumisha utamaduni wetu wa kuvaa kanga.

Kwa mtazamo wangu, maandishi ya kanga yanafundisha namna moja au nyingine, ukiyasoma kwa kina na kupata kuelewa kanga hiyo imebeba ujumbe gani.

SIRI NI YA WAWILI

UTAUMIZA ROHO YAKO

USIMLAUMU SISIMIZI SUKARI HAIMALIZI
Mbali na kuwa maandishi mengi ya kanga ni misemo ya Kiswahili, pia maandishi hayo yanaweza yakawa ni  ujumbe wa upendo, tahadhari, onyo au tu mtu binafsi kapenda kueleza anachohisi moyoni.

Monday, October 1, 2012

WAZO LA LEO

“Tambua ni nini lengo lako katika maisha na hakikisha unafuatilia mpaka unafanikisha, hakuna siri kubwa ya maendeleo.” - Richelle E. Goodrich.

Friday, September 28, 2012

WAZO LA LEO

''Mtu anayesema kitu fulani hakiwezekani, asimuingilie ama kumpinga yule ambaye anaweza kukifanya'' Unknown.

Wednesday, September 26, 2012

UZINDUZI WA EBSS HOUSE




Hafla ndogo ilifanyika kwa ajili ya kuzindua EBSS HOUSE. Washiriki 12 bora waliochaguliwa watapata fursa ya kuishi ndani ya nyumba hii hadi hapo mshindi atapo patikana.

WAZO LA LEO

Hebu jiulize, 

''Ni kitu gani kikubwa wewe ungejaribu kama ungejua kuwa huwezi kushindwa? - Robert H. Schuller''

Monday, September 24, 2012

TAMADUNI ZA WENZETU

Wanawake wa kabila la Himba lililoko nchini Zambia wanajipaka matope wanayo yaita 'Otjize' na ni kwasababu hiyo wamepewa jina la 'Red Women.'


Inasemekana matope hayo wanayapaka ili kuzuia wadudu na jua lakini wahimba wenyewe wanasema wanasababu zao muhimu zinazowafanya wapake matope hayo.
Matope haya yanapakwa na wanawake wa Himba kila waamkapo asubuhi lakini wanaume hawaruhusiwi kupaka.

WAZO LA LEO

"Ukifurahia kazi yako unaweka ukamilifu katika kazi." - Aristotle

Thursday, September 20, 2012

BEHING THE SCENE

Nikiwa napambwa na Miss Ria. Huyu mwanadada ni mtaalam wa urembo ambaye pia anawapamba washiriki wa EBSS 2012 na kuhakikisha wamependeza........

Hii ni behind the scene kabla filming ya EBSS haijaanza.

WASHIRIKI WA EBSS WAONYESHA VIPAJI VYAO

EBSS tunawakaribisha wadau wetu wote kuangalia BURE, LIVE perfomance ya Top 20 inayofanyika leo, Budget Hotel njia panda ya Bahari Beach, Kunduchi. Muda ni Saa 7:00 mchana!



 KARIBUNI SANA!!!

WAZO LA LEO

''Katika maisha, usiogope kujaribu kitu kipya''

Tuesday, September 18, 2012

NIKIONGELEA KUHUSU BSS

Nilipata fursa ya kuhojiwa na jarida la Bang Magazine. Mazungumzo yetu yalihusisha masuala yote kuhusiana na Bongo Star Search......


Kwa wale wote wenye maswali kuhusiana na EBSS, majibu mtayapata kwenye mahojiano baina yangu na Bang Magazine. Jarida hili linatarajia kuwa mtaani hivi karibuni...... Usikose kununua!

Monday, September 17, 2012

WANAWAKE NA SIASA

Miaka ya hivi karibuni, wanawake wamekuwa mstari wa mbele katika medani za siasa barani Afrika na hata wengine wakiwa wameshikilia wadha mkubwa serikalini.

Hawa ndio baadhi ya wanawake wenye nguvu kisiasa Afrika.

Ellen Johnson Sirleaf - Rais wa Liberia

Joyce Banda - Rais wa Malawi

Ngozi Okonjo-Iweala - Waziri wa Fedha, Nigeria

Luisa Dias Diogo - Aliwahi kuwa Waziri Mkuu, Mozambique
Anna Makinda - Spika wa Bunge, Tanzania

Ni umahiri wa wanawake hawa ndio unaotupa nguvu sisi kama wanawake  na kutuongezea kujiamini. 

WAZO LA LEO

"Kosa kubwa unaweza kufanya katika maisha ni daima kuogopa kwamba utafanya kosa." - Elbert Hubbard

Friday, September 14, 2012

WAZO LA LEO

''Yeyote mwenye furaha huwafanya na wenzake wawe na 
furaha pia - Anne Frank.''

Wednesday, September 12, 2012

EBSS EXCLUSIVE NDANI YA BAABKUBWA

Exclusive: EPIC BONGO STAR SEARCH....HUKU MAMBO NI MOTOO!


Baabkubwa Magazine toleo jipya linatarajia kutoka wiki hii likiwa na muonekano mpya huku ndani likiwa na line ya Zantel ambayo ina mkwanja na pia itakuwezesha kukupa nafasi ya kushindani zawadi kibao kutoka Zantel... Usikose kusoma toleo hili likiwa na habari mbalimbali kuhusiana na EBSS. 

Tuesday, September 11, 2012

KIVUTIO

Umeshapigia kura?

Mlima Kilimanjaro ni miongoni mwa vivutio kutoka Tanzania ambavyo vimeingizwa kwenye shindano la kutafuta Maajabu Saba Asilia ya Afrika (SEVEN NATURAL WONDERS OF AFRICA). Vivutio vingine kutoka nchini ambavyo pia vimetajwa kwenye shindano hilo ni pamoja na Ngorongoro Crater na Serengeti National Park.

WAZO LA LEO



''Imani inajenga uhalisia - William James''

Friday, September 7, 2012

KUTOKA FACEBOOK

Nimekutana na hii post Facebook.....



WAZO LA LEO


"Ili kuwepo na maendeleo ya ukweli na haswa yanayo onekana, ni lazima wananchi washirikishwe - Julius Kambarage Nyerere''

Wednesday, September 5, 2012

KUTOA NI MOYO





Nikikata utepe na Paschal Cassian kwa ajili ya uzinduzi
Paschal akiwa jukwaani anatumbuiza mashabiki


Martha Mwaipaja naye alitoa mchango wake jukwaani


Nilipata fursa ya kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa album mpya ya Injili ya Paschal Cassian (Mshindi wa BSS 2009) iitwayo 'Yasamehe Bure' katika hafla iliyofanyika Jumapili iliyopita. Paschal alichagua kufanya uzinduzi huo Uwanja wa Fisi, Manzese kwa nia ya kuchangisha kiasi cha millioni 30 kupitia mauzo ya album hiyo kwa ajili ya kupambana na biashara ya ukahaba inayofanywa na wasichana wa eneo hilo.

Bila kumuangusha, nami nilitoa mchango wangu ili kusaidia kufanikisha kampeni hiyo muhimu. Binafsi naamini kuwa, ili kupambana na biashara hiyo haramu inatakiwa kwanza wanaume waepukane na tabia ya kununua wasichana hao kwa kuwa wanunuzi wasipokuwepo basi hata wauzaji hawatakuwepo. 

WAZO LA LEO

''Hatuwezi kusaidia kila mtu, lakini kila mtu anaweza kumsaidia mtu--- Ronald Reagan''

Wednesday, August 29, 2012

TUONGEE FEDHA

FAHAMU MBINU ZA KUWEKA AKIBA BENKI

Kuweka akiba ya fedha ni kazi rahisi sana ambayo kila mtu anaweza kufanya pindi apatapo fedha, lakini wengi wetu inatuwia ugumu kufanya hivyo. Hamu ya kutaka kuanza kuweka akiba tunayo lakini watu wengi  hushindwa kufanya hivyo. Mara nyingi watu wanajikuta wanakabiliana na hali ambapo pale wanapohitaji fedha, wanakuwa hawana fedha yoyote ya ziada.

SASA BASI UNAANZAJE KUWEKA AKIBA?

  1. Fahamu lengo lako: Kwa nini unataka kuweka akiba ya fedha? Je, nini hasa dhumuni la kuweka akiba hiyo?
  2. Tambua ni kiasi gani unataka kuweka kando: Ukifahamu lengo la matumizi ya kiasi unachotaka kuweka akiba, utapata pia kujua ni kiasi gani unahitaji kuweka akiba kila siku, wiki au mwezi.
  3. Weka muda maalum: Baada ya kuanza kuweka akiba, jiwekee muda. Mfano; mpaka tarehe fulani nataka niwe na kiasi fulani ndani ya account yangu.
  4. Kadiria kiasi unachotaka kuwa unaweka akiba na pia tambua ni mara ngapi ungependa kuweka fedha katika account yako.



WAZO LA LEO

''Hakuna uhakika kwamba maisha haya ni rahisi''

Tuesday, August 28, 2012

FURAHA YA KUJITOLEA



Katika maisha, kila siku jaribu kumfanyia mtu mwingine kitu kizuri. Sio lazima uumpe mtu fedha, hata ukimsaidia kimawazo, kusaidia kazi za ndani au pia kumsaidia mzee au mtoto wa shule ya msingi kuvuka barabara, utakuwa umefanya kitu kizuri kwa mtu mwingine bila kutarajia malipo. Kama msemo uendao 'Tenda wema, nenda zako usingoje shukrani.'

Toa msaada kila siku uwezavyo. Mbali na hapo, unaweza ukapangilia na kuingiza kwenye ratiba yako ya kila siku kuwa utamsaidia mtu kitu fulani kwa siku hiyo. Tabia hii daima itakufanya uwe mtu mwenye amani na furaha moyoni. Jaribu kufanya hivyo kwa wiki moja halafu naomba uje utoe ushuhuda kwenye blog hii ya jinsi gani unavyojisikia vizuri!

Monday, August 27, 2012

WAZO LA LEO

''Kila kitu kina uzuri wake, lakini sio kila mtu analiona hilo - Confucius''

UBUNIFU KUTOKA AFRICA


Hii ni moja ya baiskeli zinazotengenezwa kutokana na mianzi. Baiskeli hizi zinatengenezwa na kampuni iitwayo Zambikes nchini Zambia. Zinatumiwa na watu mbali mbali wanaohitaji baiskeli kwa ajili ya kusafiri kutoka eneo moja kwenda lingine. HUU NI UBUNIFU WA HALI YA JUU ULIOTOKANA NA MAWAZO YA VIJANA AMBAO BAADA YA KUFUZU ELIMU YAO YA JUU, WALITAFUTA KAZI KWA MUDA MREFU BILA MAFANIKIO NA BADALA YA KUKATA TAMAA YA MAISHA WAKAAMUA KUJIAJIRI. Kwa habari kamili, soma hapa;
http://edition.cnn.com/2012/05/31/business/bamboo-bicycles-zambia-zambikes/index.html?iref=allsearch

WAZO LA LEO

''Ni vizuri kusherehekea mafanikio, lakini pia ni muhimu zaidi kujifunza somo la wapi ulishindwa wakati unatafuta mafaniko hayo - Bill Gates"

Friday, August 24, 2012

Nikihojiwa na ITV kuhusu EBSS wiki chache zilizopita

Naamini kuwa mtu akipewa nafasi ya kuonyesha uwezo wake aidha kimziki au kiufanisi basi achukue nafasi hiyo kuonyesha kipaji chake kwa umahiri mkubwa. Siku zote katika maisha usichukulie nafasi unayopewa kama mzaha, bali jitahidi juhudi zako zionekane.