Wednesday, August 29, 2012

TUONGEE FEDHA

FAHAMU MBINU ZA KUWEKA AKIBA BENKI

Kuweka akiba ya fedha ni kazi rahisi sana ambayo kila mtu anaweza kufanya pindi apatapo fedha, lakini wengi wetu inatuwia ugumu kufanya hivyo. Hamu ya kutaka kuanza kuweka akiba tunayo lakini watu wengi  hushindwa kufanya hivyo. Mara nyingi watu wanajikuta wanakabiliana na hali ambapo pale wanapohitaji fedha, wanakuwa hawana fedha yoyote ya ziada.

SASA BASI UNAANZAJE KUWEKA AKIBA?

  1. Fahamu lengo lako: Kwa nini unataka kuweka akiba ya fedha? Je, nini hasa dhumuni la kuweka akiba hiyo?
  2. Tambua ni kiasi gani unataka kuweka kando: Ukifahamu lengo la matumizi ya kiasi unachotaka kuweka akiba, utapata pia kujua ni kiasi gani unahitaji kuweka akiba kila siku, wiki au mwezi.
  3. Weka muda maalum: Baada ya kuanza kuweka akiba, jiwekee muda. Mfano; mpaka tarehe fulani nataka niwe na kiasi fulani ndani ya account yangu.
  4. Kadiria kiasi unachotaka kuwa unaweka akiba na pia tambua ni mara ngapi ungependa kuweka fedha katika account yako.



WAZO LA LEO

''Hakuna uhakika kwamba maisha haya ni rahisi''

Tuesday, August 28, 2012

FURAHA YA KUJITOLEA



Katika maisha, kila siku jaribu kumfanyia mtu mwingine kitu kizuri. Sio lazima uumpe mtu fedha, hata ukimsaidia kimawazo, kusaidia kazi za ndani au pia kumsaidia mzee au mtoto wa shule ya msingi kuvuka barabara, utakuwa umefanya kitu kizuri kwa mtu mwingine bila kutarajia malipo. Kama msemo uendao 'Tenda wema, nenda zako usingoje shukrani.'

Toa msaada kila siku uwezavyo. Mbali na hapo, unaweza ukapangilia na kuingiza kwenye ratiba yako ya kila siku kuwa utamsaidia mtu kitu fulani kwa siku hiyo. Tabia hii daima itakufanya uwe mtu mwenye amani na furaha moyoni. Jaribu kufanya hivyo kwa wiki moja halafu naomba uje utoe ushuhuda kwenye blog hii ya jinsi gani unavyojisikia vizuri!

Monday, August 27, 2012

WAZO LA LEO

''Kila kitu kina uzuri wake, lakini sio kila mtu analiona hilo - Confucius''

UBUNIFU KUTOKA AFRICA


Hii ni moja ya baiskeli zinazotengenezwa kutokana na mianzi. Baiskeli hizi zinatengenezwa na kampuni iitwayo Zambikes nchini Zambia. Zinatumiwa na watu mbali mbali wanaohitaji baiskeli kwa ajili ya kusafiri kutoka eneo moja kwenda lingine. HUU NI UBUNIFU WA HALI YA JUU ULIOTOKANA NA MAWAZO YA VIJANA AMBAO BAADA YA KUFUZU ELIMU YAO YA JUU, WALITAFUTA KAZI KWA MUDA MREFU BILA MAFANIKIO NA BADALA YA KUKATA TAMAA YA MAISHA WAKAAMUA KUJIAJIRI. Kwa habari kamili, soma hapa;
http://edition.cnn.com/2012/05/31/business/bamboo-bicycles-zambia-zambikes/index.html?iref=allsearch

WAZO LA LEO

''Ni vizuri kusherehekea mafanikio, lakini pia ni muhimu zaidi kujifunza somo la wapi ulishindwa wakati unatafuta mafaniko hayo - Bill Gates"

Friday, August 24, 2012

Nikihojiwa na ITV kuhusu EBSS wiki chache zilizopita

Naamini kuwa mtu akipewa nafasi ya kuonyesha uwezo wake aidha kimziki au kiufanisi basi achukue nafasi hiyo kuonyesha kipaji chake kwa umahiri mkubwa. Siku zote katika maisha usichukulie nafasi unayopewa kama mzaha, bali jitahidi juhudi zako zionekane.