Tuesday, August 28, 2012

FURAHA YA KUJITOLEA



Katika maisha, kila siku jaribu kumfanyia mtu mwingine kitu kizuri. Sio lazima uumpe mtu fedha, hata ukimsaidia kimawazo, kusaidia kazi za ndani au pia kumsaidia mzee au mtoto wa shule ya msingi kuvuka barabara, utakuwa umefanya kitu kizuri kwa mtu mwingine bila kutarajia malipo. Kama msemo uendao 'Tenda wema, nenda zako usingoje shukrani.'

Toa msaada kila siku uwezavyo. Mbali na hapo, unaweza ukapangilia na kuingiza kwenye ratiba yako ya kila siku kuwa utamsaidia mtu kitu fulani kwa siku hiyo. Tabia hii daima itakufanya uwe mtu mwenye amani na furaha moyoni. Jaribu kufanya hivyo kwa wiki moja halafu naomba uje utoe ushuhuda kwenye blog hii ya jinsi gani unavyojisikia vizuri!

2 comments:

  1. madam rita huwa nakuonaga kwenye tv kama hakimu wa bss, hata hivi nakupongeza ww na salama na master jay kwa kazi nzito na kuwasupport vijana.

    Ama kuhusu maisha na kusaidia si kila mtu anaweza fanya, u no why nasema vile ? Kuna jirani yangu ni demu huku mbezi ana gari mi sina nilishanga siku hiyo anatoka getini kwake na kaniona na kanipa haiiiiii .......nikawa namuisharia vipi lift nilishanga alivyo jikausha na kuondoa gari kusema kweli kiliniuma sana lkn nikasema ipo siku ntapata gari.
    Hi comnet nakupa mfano wa mtu na siyo wa mbali ni jirani na anajuwana na wife wangu they r friends.

    ReplyDelete
  2. Karibu katika kublog. Mimi ni young blogger pia. Najifunza vitu vizuri vya maisha toka kwako. Ni kweli unachosema. mimi na familia yangu tuna uwezo wa kawaida tu, lakini tunapenda kusaidia wengine. Na tunajiskia furaha kufanya hivi. Mungu akubariki Madam.

    ReplyDelete