Kuweka akiba ya fedha ni kazi rahisi sana ambayo kila mtu anaweza kufanya pindi apatapo fedha, lakini wengi wetu inatuwia ugumu kufanya hivyo. Hamu ya kutaka kuanza kuweka akiba tunayo lakini watu wengi hushindwa kufanya hivyo. Mara nyingi watu wanajikuta wanakabiliana na hali ambapo pale wanapohitaji fedha, wanakuwa hawana fedha yoyote ya ziada.
SASA BASI UNAANZAJE KUWEKA AKIBA?
- Fahamu lengo lako: Kwa nini unataka kuweka akiba ya fedha? Je, nini hasa dhumuni la kuweka akiba hiyo?
- Tambua ni kiasi gani unataka kuweka kando: Ukifahamu lengo la matumizi ya kiasi unachotaka kuweka akiba, utapata pia kujua ni kiasi gani unahitaji kuweka akiba kila siku, wiki au mwezi.
- Weka muda maalum: Baada ya kuanza kuweka akiba, jiwekee muda. Mfano; mpaka tarehe fulani nataka niwe na kiasi fulani ndani ya account yangu.
- Kadiria kiasi unachotaka kuwa unaweka akiba na pia tambua ni mara ngapi ungependa kuweka fedha katika account yako.